President’s Office, Constitution, Legal Affairs, Public Service and Good Governance

THE LAW SCHOOL OF ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Jijini Dodoma.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Dodoma,baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuhudhuria Uzinduzi wa Wiki ya Sheria.Inayotarajiwa kufanyika kesho 23-1-2022 Jijini Dodoma.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yatakayofanyika (23.01.2022) hapa Jijini Dodoma. Rais Dk. Mwinyi amewasili leo jioni Jijini Dodoma na ujumbe wake akiwa amefuatana na mkewe mama Mariam Mwinyi ambapo katika uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dk. Mwinyi alipokewa na viongozi wakuu wa Mkoa huo.

Maadhimisho hayo yatatanguliwa na matembezi ya kilomita saba yatakayoanzia katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Haki, Jijini Dodoma na kupita katika maeneio mbali mbali na hatimae kuishia katika viwanja vya Nyerere Squire. Kabla ya uzinduzi huo Rais Dk. Mwinyi atatembelea mabanda ya maonyesho pamoja na kuzindua bendera na Nembo ya Mahakama.